Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, August 18, 2009

ZIARA YA MKURUGENZI WA WHO NCHINI

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof.David Mwakyusa akimuuliza maswali Bi.Regina Martin mmoja wa wananchi waliofika kutibiwa baada ya kutembelea moja ya chumba cha daktari katika zahanati ya kijiji cha Mapinga wilayani Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Margaret Chan.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Mapinga wilayani Bagamoyo wakati Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Dk. Margaret Chan alipotembelea zahanati ya kijiji hicho leo kuona maendeleo na huduma mbalimbali za afya zinazotolewa.


Mkuu wa kituo cha Afya cha Ifakara kilichopo wilayani Bagamoyo Dk. Salim Ahmed akitoa maelezo kwa ugeni kutoka WHO kuhusu huduma zinazotolewa na kituo hicho leo wilayani Bagamyo.

Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dafroza Lymo akitoa maelezo kwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Margaret Chan kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo wakati alipoitembelea hospitali hiyo jana jijini Dar es salaam.Mstari wa nyuma (katikati) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa



Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Margaret Chan akimsalimia Bi.Eliza Marius na mtoto wake Pius Marius katika wodi ya watoto katika kituo cha Afya cha Ifakara Wilayani Bagamoyo




Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk .Margaret Chan akitoa maelezo kuhusiana na tiba bora na namna ya kuzuia Ugonjwa wa malaria mara baada ya kutembelea kituo cha Afya cha Ifakara wilayani Bagamoyo, Pwani.Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa.





Rais Jakaya Kikwete akimuaga Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Margaret Chan mara baada ya kuzungumza naye Ikulu ndogo, Chamwino Dodoma. Dkt Chan alirejea jijini Dar es salaam kuendelea na ziara yake.







Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Margaret Chan akipokea maelezo kutoka kwa madaktari kuhusu huduma zinazotolewa kwa akina mama na watoto katika moja ya wodi alizotembelea katika hospitali ya Amana jana jijini Dar es salaam.Dkt Chan alitembelea hospitali hiyo kujionea juhudi mbalimbali zinazofanya katika kupambana na Malaria,utoaji wa huduma ya mama na mtoto,utunzaji na utoaji wa madawa kwa wagonjwa

Picha zote na Aron Msigwa wa Maelezo




0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP