Wednesday, September 30, 2009
Discussing...
Prime Minister Mizengo Pinda chatting with the Minister for Livestock Development and Fishery,Mr John Magufuli at a meeting discussing livestock development in the country,held in Dodoma held yesterday.Photo by Prime Minister Office
MWANAMITINDO FATMA AMOUR KUZINDUA "MAGIC OF TANZANIA" NCHINI MAREKANI
Mkuu wa kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Marekani aliyekaa kulia Karen Grisette akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ubalozi huo leo wakati alipowatangaza Wanawake watanzania 13 wanaotarajia kwenda nchini humo kwa mafunzo mbalimbali ya kazi za sanaa kwa mwezi mmoja, hili ni kundi la tatu kwenda nchini Marekani kwa mafunzo hayo makundi mengine mawili yameshakwenda na kupata mafunzo na wamerejea nchini.
Karen amesema wasanii hao kutoka mikoa ya Tanga, Zanzibar Bagamoyo Dar es salaam Arusha na Dodoma watashiriki katika maonyesha ya sanaa za aina mbalimbali yanayoandaliwa na vikundi vya sanaa vya Jimbo la Ohio nchini humo.
Ameongeza kuwa mafunzo yataanza tarehe 6 oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba ambapo mpango huu wa mafunzo unadhaminiwa na serikali ya Marekani, ameongeza kuwa wasanii hawa pia watatembelea jumuiya mbalimbali katika majimbo ya Michigan na Ohio,
Katika safari hiyo Mwanamitindo mbunifu wa Tanzania Fatma Amour Hamad wa Famour Designs ambaye ataongoza wenzake 12 katika safari hiyo anatarajiwa kuzindua mitindo yake katika hafla ya uchangiaji wa sanaa yenye jina "Magic Of Tanzania" uzinduzi utakaofanyika jimbo la Ohio tarehe 12 oktoba, pia atatambulisha mitindo na kazi zake nyingine za sanaa katika maonyesho mengine nchini Marekani.
Fatma Amour akitoa shukurani zake kwa Ubalozi wa Marekani kwa kumchagua kwenda katika mafunzo hayo yatakayochukua mwezi mmoja nchini Marekani.
kutoka kushoto ni Fatma amour,Zena Abdallah,Amoke Kyando aliyerejea kutoka katika mafunzo hayoSalma Masenga, Harieth Kagangule, Mwandale mwanyekwa (Big Mama) na Scolastca Malecela wakiwa katika picha ya pamoja
Read more...Mama Kikwete Twiga sekondari.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua Maabara ya Komputa katika shule ya Sekondari ya Twiga wakati wa mahafali ya kwanza shuleni hapo juzi.
iliyopo Tegeta Dar es Salaam
Tuesday, September 29, 2009
Ajinyakulia Nokia E-66 na tuzo, baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Gofu
Mambo ya uzinduzi wa michuano ya Netiboli
Katibu mkuu msaidizi wa CHANETA Rose Mkisi kushoto na Mweka hazina wa chama hicho Flora Kasambara wakiingia katika viwanja vya mashindano kabla ya kufunguliwa rasmi na mke wa rais Mama Salma Kikwete jana
Mke wa Rais Mama Salama Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya netball kwenye uwanja mkuu wa Taifa jana akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho ambapo Tanzania ilishinda magoli 33-19 mashindano hayo ya kimataifa ya Netball yanasimamiwa shirikisho la vyama vya Netball vya kimatifa International Federation of Netball Association (IFNA)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati alipofungua mashindano ya Netball kwa nchi za Afrika yanayofanyika nchini yakiandaliwa na chama cha Netball CHANETA yaliyoanza jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa. kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama na anayefuata ni Anna Bayi Mwenyekiti wa Chama cha hicho.
JK afungua jengo la ubalozi wetu Washington DC
Jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani ambalo JK alilifungua jana asubuhi. Jengo hili limenunuliwa na serikali ya Tanzania kwa jumla ya dola za kimarekani $10,415,000.
JK akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani jana asubuhi
JK akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijinji Washington Marekani jana asubuhi.
JK akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Balozi iliyopo katika jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani jana asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na wapili kushoto ni Balozi wa Tanzania Washington Ombeni Sefue
Picha na Freddy Maro wa Ikulu
Barack Obama and First Lady Michelle Obama With World Leaders at the Metropolitan Museum in New York
President Barack Obama and First Lady Michelle Obama pose for a photo during a reception at the Metropolitan Museum in New York with H.E. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Deputy Secretary-General of the United Nations, Wednesday, Sept. 23, 2009. (Official White House Photo by Lawrence Jackson)
President Barack Obama and First Lady Michelle Obama pose for a photo during a reception at the Metropolitan Museum in New York with H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, Wednesday, Sept. 23, 2009. (Official White House Photo by Lawrence Jackson)
Vyoo vya kikohozi.
Ukitaka kujua kama kuna mtu anatumika humu ndani basi we kohoa tu na utapata majibu, lakini hii ni maalum kwa wliopitia mazingira kama haya.
Viongozi wetu wametokea huku lakini leo hii ni mafisadi wakubwa na wanasahau walikotoka na waliowaacha nyuma yao.
Maria Nyerere azungumza na waandishi
Monday, September 28, 2009
Wanafunzi Kibasila Sekondari wafunga Barabara
WANAFUNZI wa shule ya sekondari kibasila na shule ya msingi kibasila leo walikua na mgomo kutokana na eneo hilo kuwa na ajali za mara kwa mara kusababisha vifo kwa wanafunzi wa shule hizo.
Rais Kikwete akutana na Ban-ki-Moon New York
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika mkutano na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-ki Moon na ujumbe wake katika ofisi yake iliyopo ndani makao makuu ya Umoja wa Mataifa(UN) jijini New York mapema jana asubuhi
Afunga Ndoa na Wanawake Wanne Kwa Mpigo
Miss Utalii Temeke 2009- Erica Allan (kati), wa pili Mariam Khamis(kushoto) na 3-Zainabu Matagi-
Mbunge wa Temeke ,Abbas Mtemvu & Mariam Mtemvu, wakishuhudia fainali za shindano la Miss Utalii Temeke 2009, City Garden usiku wa kuamkia jumamosi
Saturday, September 26, 2009
JK Na Kamaresh New York
JK na Ray chambers wa mumbe maalum wa malaria
Ajali zaingine jamani!!!
TBL yaipiga jeki kamati ya usalama barabarani
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Maneno Mbegu (kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 800, Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, James Kombe, ikiwa ni msaada kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama itakayoadhimishwa mkoani Mbeya kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 3, Mwaka huu. Katika hafla hiyo iliyofanyika Dar leo, TBL walikabidhi pia msaada wa stika 4000, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 10.
Friday, September 25, 2009
BASKETBALL CHARITY DAY
Jaji Mkuu wa Tanzania na Mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini TBF Jaji Augustino Ramadhan akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo asubuhi wakati alipotangaza maandalizi ya bonaza la mpira wa kikapu lililopewa jina la "BASKETBALL CHARITY DAY" litakalofanyika kuanzia oktoba 17 mpaka 22 na kuhitimishwa tarehe 24 kwa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa viwanja zaidi ya vitano nchini kote huku mgeni rasmi akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete, jumla ya shiligi milioni 10 zinatarajiwa kukusanywa katika Harambee hiyo , wanaofuata katika pisha ni Lawrence Cheyo Katibu mkuu wa TBF na Saimon Msofe Mwenyekiti wa caha cha Basketball jijini Dar es salaam (DABA). Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF Lawrence Cheyo akimkaribisha Mlezi wa shirikisho hilo Jaji mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhan wa pili kutoka kulia wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar, anayefuatia ni Eke Mwaipopo mchezaji wa zamani mpira wa kikapu na mwenyekiti wa kamati ya tamasha la kikapu linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
JAPAN YATOA BILIONI 2.4 KUSAIDIA MPANGO WA KUDHIBITI UKIMWI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akibadilishana hati na Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa jijini leo kuhusu msaada wa fedha wenye thamani ya bilioni 2.4 za kitanzania kwaajili kununulia madawa na vitendea kazi muhimu katika mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi.( 2.4 billion for procerement of equipment, medicines and services necessary for implementing the HIV/AIDS Control programme mara baada ya kusaini hati hizo hafla ya kusaini hati hizo imefanyika katika Wizara ya Fedha na Uchumi.(Picha na Mwanakombo Jumaa wa Maelezo).
Miss Tanzania ndani ya Vodashop
Dar es salaam.
USAID YAMWAGA VIFAA VYA KUPIMIA KIFUA KIKUU
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni akiangalia kifaa cha kupimia ugonjwa ya kifua kikuu (Microscope) iliyokabidhiwa kwake na Elise Jensen (wa kwanza kulia) mwakilishi wa shirika la misaada la Marekani (USAID) huku maofisa wa Wizara na shirika la USAID wakishuhudia, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Wizara ya Afya. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Microscope 40, Jokofu moja na microscopy slide boxes 1600 vyote vikiwa na thamani ya dola za Kimarekani 109,715 na vitagawanywa katika mikoa yote nchini.