MWANAMITINDO FATMA AMOUR KUZINDUA "MAGIC OF TANZANIA" NCHINI MAREKANI
Mkuu wa kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Marekani aliyekaa kulia Karen Grisette akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ubalozi huo leo wakati alipowatangaza Wanawake watanzania 13 wanaotarajia kwenda nchini humo kwa mafunzo mbalimbali ya kazi za sanaa kwa mwezi mmoja, hili ni kundi la tatu kwenda nchini Marekani kwa mafunzo hayo makundi mengine mawili yameshakwenda na kupata mafunzo na wamerejea nchini.
Karen amesema wasanii hao kutoka mikoa ya Tanga, Zanzibar Bagamoyo Dar es salaam Arusha na Dodoma watashiriki katika maonyesha ya sanaa za aina mbalimbali yanayoandaliwa na vikundi vya sanaa vya Jimbo la Ohio nchini humo.
Ameongeza kuwa mafunzo yataanza tarehe 6 oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba ambapo mpango huu wa mafunzo unadhaminiwa na serikali ya Marekani, ameongeza kuwa wasanii hawa pia watatembelea jumuiya mbalimbali katika majimbo ya Michigan na Ohio,
Katika safari hiyo Mwanamitindo mbunifu wa Tanzania Fatma Amour Hamad wa Famour Designs ambaye ataongoza wenzake 12 katika safari hiyo anatarajiwa kuzindua mitindo yake katika hafla ya uchangiaji wa sanaa yenye jina "Magic Of Tanzania" uzinduzi utakaofanyika jimbo la Ohio tarehe 12 oktoba, pia atatambulisha mitindo na kazi zake nyingine za sanaa katika maonyesho mengine nchini Marekani.
Fatma Amour akitoa shukurani zake kwa Ubalozi wa Marekani kwa kumchagua kwenda katika mafunzo hayo yatakayochukua mwezi mmoja nchini Marekani.
kutoka kushoto ni Fatma amour,Zena Abdallah,Amoke Kyando aliyerejea kutoka katika mafunzo hayoSalma Masenga, Harieth Kagangule, Mwandale mwanyekwa (Big Mama) na Scolastca Malecela wakiwa katika picha ya pamoja
0 comments:
Post a Comment