Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, September 29, 2009

Mambo ya uzinduzi wa michuano ya Netiboli

Katibu mkuu msaidizi wa CHANETA Rose Mkisi kushoto na Mweka hazina wa chama hicho Flora Kasambara wakiingia katika viwanja vya mashindano kabla ya kufunguliwa rasmi na mke wa rais Mama Salma Kikwete jana


Mke wa Rais Mama Salama Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya netball kwenye uwanja mkuu wa Taifa jana akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho ambapo Tanzania ilishinda magoli 33-19 mashindano hayo ya kimataifa ya Netball yanasimamiwa shirikisho la vyama vya Netball vya kimatifa International Federation of Netball Association (IFNA)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati alipofungua mashindano ya Netball kwa nchi za Afrika yanayofanyika nchini yakiandaliwa na chama cha Netball CHANETA yaliyoanza jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa. kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama na anayefuata ni Anna Bayi Mwenyekiti wa Chama cha hicho.


Kuazia kushoto ni Timu za Tanzania, Namibia na Afrika kusini zikiwa zimekaa tayari kwa kupigiwa nyimbo za mataifa yao wakati wa ufunguzi wa mashindano ya NetBall kwa nchi za Afrika jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa.





Mchezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Queen akijaribu kufunga goli katikati ya walinzi wawili wa timu ya Lesotho wakati wa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa mashindano hayo ya Mchezo wa Netball kati ya timu hizo iliyofanyika jana kwenye uwanja mkuu wa taifa Tanznia ilishinda magoli 33-19.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP