JET YAWATUNUKU VYETI WAANDISHI WA MAZINGIRA MIKOA YA KUSINI MWA TANZANIA.
Wahitimu wa mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira mikoa ya kusini mwa Tanzania ,Iringa,Mbeya ,Ruvuma na Rukwa wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wa mazingira nchini Tanzania (JET) Deo Mfugale (wa tano kuli) na afisa elimu mazingira wa WWF Mwamini Masanja kushoto kwake mara baada ya kutunukiwa vyeti
Afisa mazingira wa WWF Iringa Mwamini Masanja (kulia) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira mwandishi wa mwananchi Mbeya Blandina Nelsoni ,anayeshuhudia ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa mazingira nchini (JET) Deo Mfugale.
Afisa mazingira wa WWF Iringa Bibi Mwamini Masanja (kulia) akimtunuku cheti mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Bw Francis Godwin mara baada ya kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira yaliyoendeshwa na chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) na British High Commission jijini Mbeya ,wanaoshuhudia ni mwenyekiti wa JET Deo Mfugale na mwandishi wa Mtanzania Ruvuma Happy Kulanga ambaye pia alikuwa mhitimu
Mwandishi wa habari wa Nipashe Mbeya Thobias Mwanakatwe akikabidhiwa cheti chake baada ya kuhitimu mafuno ya uandishi wa habari wa mazingira
Mwandishi wa Uhuru na Mzalendo Ruvuma Bw Dastany Ndunguru akitunukiwa cheti cha JET
Happy Kulanga (kushoto ) ni mwandishi wa Mtanzania aliyetunukiwa cheti cha uandishi wa habari za mazingira nchini baada ya kupata mafunzo na kuelewa vyema juu ya mazingira.
Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin wa Iringa
0 comments:
Post a Comment