Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, September 28, 2009

Afunga Ndoa na Wanawake Wanne Kwa Mpigo


Mwanaume mmoja wa nchini Afrika Kusini ambaye ana mke na watoto 11 amejipatia umaarufu wa ghafla duniani baada ya kufunga ndoa na wanawake wanne kwa mpigo.Bwana harusi Milton Mbhele aliwasili kwenye harusi yake jumamosi akiwa kwenye gari jeupe aina ya limousine akiwa pamoja na mabibi harusi wake wanne.Mabibi harusi wote wanne walivalishwa pete za ndoa na kupigwa busu la nguvu na bwana harusi Mbhele katika harusi kubwa ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na mamia ya watu.Sheria za Afrika Kusini zinaruhusu ndoa za wake wengi hata rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ana wake watatu. Utamaduni wa wake wengi ni wa kawaida katika makabila ya Zulu na Swazi.Hata hivyo ni mara chache sana hutokea mwanaume akafunga ndoa na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP