Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, September 25, 2009

EABL yaisaidia Hospitali ya KCMC Moshi

Kampuni ya bia ya East African Breweries Limited EABL iliyoko nchiniKenya imejengakitengo cha huduma ya macho katika hospitli ya rufaa yaKCMC ambacho kitagharimu zaidi ya shilling million 150 hadi kukamilika.
Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa jingo hilo Mkurugenzi wa Idaraya huduma wa kampuni hiyo bwana Ken Kariuki alisema kampuni hiyo iliamuakujenga kitengo hicho baada ya kufika katika hospitali hiyo na kukutahaina kitengo cha macho.
Bwana Kariuki alisema jingo hilo ambalolimeanza kujengwa miaka miwili iliyopita wanatajia kulimaliza mwezioctoba mwaka huu na watalikabidhi kw wahusika ili wananchi wa moshi namaeneo jirani ya nje na ndani ya nchi waweze kunufaika na huduma yamacho.
Kampuni yetu hujishughulisha sana na mambo mbalimbali ya kusaidia jamiiikiwa ndio njia mojawapo ya kurudisha faida tunayoipata kutoka kwawananchi, na ndipo tulipoamua kuja kuuliza wananchi wa mkoa waKilimanjaro kuwa wanahitaji nini na walisema wanakabiliwa na tatizo lakitengo cha macho katika hospitali hiyo, alisema Bwana Kariuki.
Katika ukaguzi wa mradi huu alikuwepo pia na Mkuu wa mkoa wa KilimanjaroBibi Monica Mbega naye aliishukuru sana kampuni hii ya bia ya Africa Mashariki kwa kuwa mbele kuisaidia jamii kwa kujenga wodi ya macho nakuendeleza miradi ya maji kama vile ule mradi wa Mkuranga ambaoumeigharimu EABL kiasi cha million 350 na mradi huu umeweza kusaidiazaidi ya kata 11 na watu zaidi ya 300,000 wamefaidika.



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP