Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, September 18, 2009

Dr. Kamala alipotembelea kiwanda cha East African Cable

Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (katikati aliyevaa koti yeupe) akipata maelekezo kutoka kwa Muriithi Ndegwa ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha East African Cable (kulia kwa waziri) kuhusu roll ya waya wa shaba ambayo inaingizwa katika mashine na kutolewa katika ukubwa wa aina tofauti wa nyaya. Kulia ni Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda akifuatiwa na Joseph Kamau Meneja wa uzalishaji. Waziri huyo alitembelea kiwanda hicho leo kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki. (Picha na Anna Nkinda Maelezo)







Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (wa pili kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda cha East African Cable kuhusu mtambo wa kutengeneza nyaya za kusukia motor na transfoma wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Joseph Kamau Meneja uzalishaji akifuatiwa na Muriithi Ndegwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda. Waziri huyo alitembelea kiwanda hicho jana kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki.














0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP