Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani Duniani yafanyika viwanja vya Mnazi Mmoja leo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi mpira mwanafunzi wa shule ya msingi Mbagala wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani. Jumla ya mipira 50 ilitolewa na Right to play kwa wanafunzi walioshiriki mashindano mbalimbali. Kabla ya maadhimisho ya siku siku hiyo kulikuwa na mashindano ya mpira wa mistari yaliyozikutanisha timu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam huku ujumbe wa mwaka huu ukiwa ni silaha ziwekwe chini ili kuleta amani Duniani.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari na Msingi za jijini Dar es Salaam wakipita na mabango yenye ujumbe unaohusu amani mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Balozi Khamis Kagasheki (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja huku ujumbe wa mwaka huu ukiwa ni silaha ziwekwe chini ili kuleta amani Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja wakiangalia picha mbalimbali katika banda la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam huku ujumbe wa mwaka huu ukiwa ni silaha ziwekwe chini ili kuleta amani Duniani.
0 comments:
Post a Comment