Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, September 15, 2009

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lamuenzi Mwalimu Nyerere


Mama Maria Nyerere akivishwa na Rais wa Baraza Kuu la 63 la Umoja wa Mataifa, Father Miguel d' Escoto Brockman kwa niaba ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere tuzo maalum ya ' World Hero of Social Justice' ambayo Rais huyo amemtunuku Baba wa Taifa kwa kutambua mchango wake katika kutetea na kupigania haki na usawa kwa watu wanyonge, hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Jiji New York, Marekani na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika na mabara mengine wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa. kushoto ni balozi wa tanzania katika umoja wa mataifa, Augustine Mahiga


Mama Maria akiwa na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa walioshiriki hafla ya kukabidhiwa Tuzo kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo ilipopekelewa na Mama Maria Nyerere tuzo hiyo ya ' World Hero of Socia Justice' imetolewa na Rais wa Baraza Kuu la 63 la Umoja wa Mataifa, Miguel d' Escoto Brockman




Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, father Miguel d' Escoto Brockama akimwonyesha Mama Maria Nyerere, medali ya dhahabu ambayo rais huyo ameitengeneza maalum na kumtuza Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere. Mama Maria Nyerere alipokea Tuzo hiyo ya 'World Hero of Social Justice' kwa niaba ya Baba wa Taifa katika hafla iliyofanyika mwisho mwa wiki jijini New York, Marekani na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa Afrika na mabara mengine wanaoziwakilisha nchi zao katika umoja wa mataifa, watoto wawili wa Baba wa taifa Bw. Andrew Nyerere na Bi. RoseMary Nyerere walihudhuria hafla hiyo, kushoto ni balozi wa tanzania katika umoja wa mataifa, Augustine Mahiga na kulia ni mwenyekiti wa kundi la nchi za Afrika balozi Mourad Benmehidi kutoka Algeria


Rais wa baraza kuu la 63 la Umoja wa mataifa, father Miguel d' Escoto Brockman, akitoa maelezo kwa Mama Maria Nyerere kuhutu tuzo ya 'World Hero of Social Justice' ambayo rais huyo ametunuku Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere katika hafla iliyofanyika jijini New York, Marekani na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimal mbalimbali kutoka nchi za Afrika na mabara mengine wanaoziwakilisha nchi zao katika umoja wa mataifa



Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania nchini Marekani, Brazil na Umoja wa mataifa nao walikuwapo kumpa Tafu Mama katika hafla hiyo kutoka kulia Joram Biswalo (Brazil) Omben Sefue ( Washngton ) Tuvako Manongi ( ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa) na mwenyeji wao Augustine Mahiga (Umoja wa Mataifa) katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere





Mama Maria Nyerere katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. aliyekaa mbele na Mama Maria ni Balozi Augustine Mahiga



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP