Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, September 15, 2009

Zain yafuturisha watoto yatima Zanzibar

Waziri wa Kazi, Vijana, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Asha Abdallah Juma (kulia) akimlisha futari mtoto Fatma Salum wakati wa futari iliyoandaliwa na Zain mwishoni mwa wiki kwa watoto yatima mjoni Zanzibar mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Zain kutoa futari katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa watoto yatima nchini. Pamoja nae ni wafanyakazi wa Zain Zanzibar, Mtumwa Zidiheri (katikati) na Mariam Yusuph (kulia).




Baadhi ya Wafanyakazi wa Zain Zanzibar (kushoto na nguo za pink) na Waziri wa Kazi, Vijana, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Asha Abdallah Juma (hijabu ya nyano) na Mbunge wa Viti maalum, Al-Sheymaa Kwegir (hijabu nyeupe), wakifuturu pamoja na watoto yatima mjini Ungija katika futari iliyoandaliwa na Zain mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Kazi, Vijana, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Asha Abdallah Juma, akimkabidhi gunia la mchele Talib Machano baada ya Madrasa yao ya Nuria kuibuka mshindi katika shindano la kuhifadhi Koran. Hafla hiyo iliyodhamini na Zain Tanzania ilifanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Bwawani Zanzibar ambapo Zain pia ilifuturisha watoto yatima. Katikati ni Mratibu wa Zain wa Kuendeleza Biashara Zanzibar, Dominick Coy na kulia ni Mkurugenzi wa Chuchu Radio, Yusuph Chuchu.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP