Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, February 16, 2010

Ally Rhemtulla na Zain wazindua mfuko wa kuchangia elimu wilaya Kisarawe

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi. Khanifa Karamagi (wa kwanza kutoka kushoto) akitoa hotuba yake katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe.

Bango linalomuonyesha Ally Rhemtullah ambaye ameamua kujiunga katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe kwa njia ya kufanya Fashion Show aliyoipatia jina la 'Fashion For Education Benefit'.

Mbunifu wa Mitindo, Ally Rehmtullah (pili kutoka kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya Kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe. Wa kwanza kulia ni Prof. Emmanuel Bavu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Harambee Kisarawe, Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi. Khanifa Karamagi pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza. Ufunguzi wa Kampeni hiyo umefanyikia katika hoteli ya Double Tree iliyoko Masaki jijini Dar mapema leo asubuhi.
Mwaka 2008 Wialaya ya Kisarawe ilikuwa na Shule za kata 11, ikilinganishwa na shule 6 zilizokuwapo mwaka 2006. Hata hivyo pamoja na ongezeko hilo shule 11 zilidhihirika kuwa na mapungufu kama ifuatavyo:-
1. Uhaba wa madarasa.
2. Uhaba wa nyumba za walimu na chache zilizopo kutokufikia viwango stahiki.
3. Kutokuwepo mifumo ya maji na umeme.
4. Shule zote kutokuwa na maabara.
5. Wanafunzi kutembea umabli mrefu kutoka majumbani kwao au kulazimika kupanga katika nyumba za jamii inayozunguka shule kwa kuwa hakuna hosteli mashuleni.
Mapungufu yote yaliyoorodheshwa pamoja na mengine yalithibitika kurudisha nyuma juhudi za kuimarisha elimu na maendeleo ya wilaya kwa ujumla.
Ili kuepuka hali hiyo, mapema mwaka 2008 uongozi wa wilaya uliona umuhimu wa kuhakikisha wilaya inazindua na kubuni mpango mkakati wa kushirikisha wilaya inazinduka na kubuni mpango mkakati wa kushirikisha wananchi wa Kisarawe walio ndani na nje ya wilaya, marafiki na wadau mbali mbali kuchanga kwa hali na mali ili kuboresha miundo mbinu katika shule zote za kata na kujenga chuo kimoja cha ufundi.
Mpaka sasa jumla ya michango yote ni Tsh. 29, 285,200/= ahadi ni
Tsh. 25, 174,500/= na USD 50,000/= pamoja na eneo la ekari 98 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi lililotolewa na mwananchi mmoja wa Wiraya ya Kisarawe.
Kwa wale wateja wa mtandao wa Zain jinsi ya kuchangia 'Unatuma ujumbe mfupi wenye neno ELIMU kwenda namba 15620 ambapo kampeni hii itaanza rasmi 1st March 2010 na kila SMS utakayotuma utakatwa shilingi 250/=. Pia kwa wale wanaotumia huduma ya ZAP wanaweza kuchangia kwa kutumia hiyo namba ila kima cha chini ni shilingi 1000/=






0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP