Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, February 22, 2010

TANZANIA YASHIRIKI MAONYESHO YA UTALII NCHINI ITALY

Picha hii inaonyesha ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Ezekiel Maige wa pili kushoto pamoja na ujumbe mzima wa Tanzania. Katika picha hii kuna Mkurugezi wa Bodi ya Utalii Mr Deogratius Mtukamazina na Mkuu wa Masoko Bodi ya Utalii Mr Geofrey Meena na watanzania wengine wa sekta binafsi pamoja na wawakilishi toka TANAPA, Ngorongoro na Ubalozi wa Tanzania nchini Italy.
Ambapo kwa mara nyingine Tanzania imeshiriki kwenye maonyesho ya Utalii nchini Italy yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Maonyesho yalifanyika katika jiji la Milan Italy kuanzia tarehe 18 Feb mpaka 21 Feb 2010.
Msafara wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Ezekieli Maige. Jumla ya makampuni binafsi 6, Tanapa na Ngorongoro walihudhuria maonyesho haya. Nchi ya Italy ni ya tatu katika kuleta watalii wengi wanaotenbelea nchini Tanzania na wataliano wengi hupenda kutembelea Zanzibar, Mafia, na kwenye Mbuga za Wanyama.
Hivi sasa Tanzania kupitia Bodi yake ya Utalii TTB na Wizara ya Maliasili na Utalii na Balozi mbalimbali za Tanzania iko kwenye mkakati mkubwa wa kuutangaza utalii wake katika mataifa mbalimbali ili kuweza kuongeza kiwango cha watalii kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania na imekuwa ikishiriki katika maonyesho mbalimbali ya Utalii ya kimataifa yanayofanyika Ulaya na MarekaniTanzania inaweza kufanikiwa zaidi iwapo itajiimarisha zaidi katika sekta ya Utalii kwani ni moja ya nchi zenye vivutio vingi na vilivyoorodheshwa katika maajabu saba ya Dunia, hivyo ni jukumu la watanzania pamoja na Taasisi zote zinazohusika na utalii kusimamia vyema na kuutangaza utalii wa Tanzania ili uweze kuingiza pato kubwa la fedha za kigeni na kukuza uchumi wa nchi.


Timu toka Tanzania wakiwa na picha ya pamoja na Mheshimiwa Waziri Mdogo wa Maliasili na Utalii Mhe Ezekiel Maige. Mbele yao ni bango linalowakaribisha waitaliano watembelee Tanzania wakati wa mashindano ya World Cup South Africa

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP