Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, February 22, 2010

Dk Shein ziarani Ruvuma



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makita Wilayani Mbinga baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara ya Shule hiyo leo ambapo ameahidi kuchangia jumla ya kompyuta mbili. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein katikati, akitembelea Shamba la Uzalishaji wa Mbegu bora za Mahindi linalomilikiwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT katika kijiji cha Mlale Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi na Wakulima wa kijiji cha Kitai Wilayani Mbinga aliposimama kwa muda kwa ajili ya kusalimiana na Wananchi hao, alipokuwa akielekea katika kijiji cha Makita kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari Makita leo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa Miradi ya maendeleo.


Mbunge wa Jimbo la Peramiho CCM Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma Mhe. Jenista Muhagama, akijumuika na wasanii wa ngoma ya Wazee wa jimbo hilo ambayo ni ngoma ya asili ya kukaribisha wageni Mashughuri, wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili Wilayani Mbinga kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani hum leo. Picha na Amour Nassor







Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Mlale Wilayani Mbinga, mara baada ya kuwahutubia kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika kijiji hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa Miradi ya Maendeleo.





0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP