Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, February 22, 2010

BENKI YA NBC YATOA ZAWADI KWA WIZARA YA M. JAMII

Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi, Benki ya NBC leo hii imekabidhi jumla ya Tshirts 500 kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mhe.Margaret Sitta kwa ajili ya kufanikisha Maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yanafanyika Kitaifa Mkoani Tabora.Kaulimbiu ya mwaka huu ni; "Miaka 15 Baada ya Beijing: Wanawake Wanaweza,Wapewe Nafasi".Katika picha wa pili kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe. Margaret Sitta, Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Habari wa Benki ya NBC Bw. William Kalaghe , Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi Mariam Mwaffisi, Kulia ni Bi. Robi Noella Matiku Mtaalamu wa mawasiliano wa Beki ya NBC(Hanbari, picha na Asteria Muhozya)

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP