Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Friday, February 19, 2010

Mo apata wageni Ofisini kwake.


Mbunge wa Jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji akipozi kwa picha na mgeni wake mwanamuziki Lady Jay Dee wakati mwanamuziki huyo alipomtembelea ofisini kwake katika jengo la PPF Tower jijini Dar es salaam leo, haikufahamika walizungumzia ni lakini mbunge Mohammed Dewji amekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya umasikini kupitia katika jimbo lake la Singida mjini kwa kujenga Shule, vituo vya afya na Miradi ya Maji.
Mwanamuziki Lady Jay Dee pia amekuwa akipambana vilivyo katika kuhakikisha watoto yatima nao wanaangaliwa kama walivyo watoto wengine wenye wazazi hasa baada ya kuandaa onyesho la muziki na kusherehekea sikukuu ya Christmass na watoto yatima kwenye ukumbi wa Zhonghua Victoria jijini Dar es salaam mwishoni mwa mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP