Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Thursday, February 18, 2010

Prof. Mwandosya akagua miradi ya maji Kibaha

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya na Mbunge wa Kibaha Vijijini Ibrahim Msabaha wakimsikiliza mkazi wa Kibaha Vijijini alipokuwa akitoa maelezo jana wakati Waziri Prof. Mwandosya alipofanya ziara ya kutembelea Miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Soga -Kibaha ambapo pia alitembelea shule ya sekondari ya Rafsanjani na kuongea na wanafunzi wa shule hiyo wanafunzi hao walimsomea risala yao kuhusu kero ya maji shuleni hapo.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya (kulia) akiwatambulisha maafisa wajenzi wa mradi huo wa maji wa kampuni ya CHINA ANNENG CONSTRUCTION CORP. (CCACC) jana kwa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya Halmashauri Wilaya ya Kibaha kata ya Soga.Pichani alivaa kofia ni CAO Yang .na mwengine ni WANG FEI.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP