MZUNGU KICHAA ALIZIMA TAMASHA LA BUSARA KWA MBWEMBWE
Mzungu Kichaa pia ni fundi wa kuling'uta gitaa la sollo na mwanamuziki wa kigeni anayekiwakilisha vyema kiswahili kutokana na jinsi anavyoimba , hapa anaonekana kufanya mambo makubwa wakati wa maonyesho ya mwishoni mwa tamasha hili la busara lililomalizika jana Mjini Zanzibar na ametokea kupendwa na watu wengi katika tamasha hilo kutokana na kuimba kiswahili kwa ufasaha na kuwakuna zaidi mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo wakati mwingine unapomuona akiimba huwezi amini kama jamaa ni mzungu, Mzungu Kichaa ni mmoja wa wasanii wakubwa hapa asili yake ni kutoka Nchini Denmark lakini maisha yake yote amekulia hapa Tanzania
0 comments:
Post a Comment