Dr. Salim Ahmed Salim amlilia Balozi Mwakawago.
Dk.Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), sasa AU, akizungumza na waandishi habari kufuatia kifo cha aliyekuwa balozi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Hayati Daudi Mwakawago (71).
Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) sasa AU, Dk.Salim Ahmed Salim, akitia saini kitabu cha maombolezo, kufuatia kifo cha balozi wa zamani wa kudumu wa Umoja wa Mataifa, Alhaj Daudi Mwakawago nyumbani kwa marehemu Msasani Maduka Mawili jijini Dar es Salaam Alhamisi Februari 25, 2010.
Marehemu balozi Mwakawago amefariki mapema Alfajiri ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 71.
Kwa mujibu wa mdogo wa Marehemu Yasini Mwakawago, marehemu alifia hospitali ya Aga Khan alikokimbizwa kwa kusumbuliwa na Malaria lakini baadae aligundulika kuwa na matatizo ya Figo lililopelekea apumuwe kwa taabu.
Mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumamosi Februari 27. (Picha na Khalfan Said)
0 comments:
Post a Comment