TBL YAFUNGA NDOA YA MIAKA 3 NA MISS TANZANIA
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga na Meneja wa kinywaji cha Redds Kabula Nsimo wakibadilishana Nyaraka mara baada ya kusaini mkataba huo, ambapo kampuni ya Tanzania Breweries Ltd imetiliana saini ya mkataba wa shilingi milioni 200 kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa miaka mitatu mfurulizo, wanaoshuhudia katikati kulia ni Emillian Rwejuna Meneja Udhamini wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo na kushoto ni George Kavishe Meneja Udhamini na Matukio wa Tanzania Breweries Ltd, Redds watasaidiana na issamichuzi.blogspot.com kutafuta Miss Photogenic katika shindano hilo la Miss Tanzania 2009, tukio hilo limefanyika katika Hoteli ya City Paradise kwenye klabu yake ya Savanna Lounge.
0 comments:
Post a Comment