Tamasha la jinsia lazinduliwa

Mmoja wa wasanii mahiri wa kughani mashairi hapa bongo anayetambulika kwa jina la Mrisho Mpoto alikuwepo kufikisha ujumbe kwa jamii katika tamasha hilo la jinsia,ambapo meza kuu ikiwa imeambatana na mgeni rasmi iliburudika vilivyo kwa nyimbo kadhaa zilizokuwa zikiimbwa.
Mgeni rasmi wa tamasha hilo kutoka chuo kikuu cha makerere Uganda ,Prof.Silvia Tamale,akizungumzia kwa kina juu ya mada kuu ya tamasha ambayo ni rasilimali ziwanufaishe wanawake,aidha katika mazungumzo yake aligusia pia kuhusu wanawake wengi wanaofanya biashara ya ngono kuwa wanafanya hivyo sio kwa kuchagua,bali ni kutokana na mahitaji ya kiuchumi,amebainisha kuwa sheria zilizopo zinaweka taswira kwamba hawana maadili mema,na adhabu zinalenga tu wale wanaouza,wanaonunua ngono hawaadhibiwa.Kwa nini jamii inaamua kumwadhibu tu yule anayeuza,na inamwacha mnunuzi ?
Wageni waalikwa mbalimbali walikuwepo kwenye tamasha hilo,ambalo limewajumuisha wanaharakati mbalimbali,ambao wanaendelea kujadili mada mbali mbali zilizoandaliwa na wanaharakati wenyewe kuhusu jamii nzima.
Mkurugenzi wa TGNP Bi Usu Malya akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tamasha hilo,mara baada ya kuzinduliwa rasmi na mwenyekiti wa taasisi hiyo ya TGNP,Bi Ruth Meena(haonekani pichani),tatu kulia ni mgeni rasmi wa tamasha hilo kutoka chuo kikuu cha makerere Uganda ,Prof.Silvia Tamale




0 comments:
Post a Comment