Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, March 23, 2010

Mawakala katika semina

Mgeni Rasmi katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Helmas Mwansoko akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga kushoto na Katibu mkuu Miss Tanzania Bosco Majaliwa wakiingia kwenye ufunguzi wa semina hiyo





Mkurugezi wa Utamaduni Wizara ya Habari na Utamaduni Hlmas Mwansoko akiongea katika semina ya Mawakala wa Miss Tanzania kwa mikoa yote ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza leo kwenye Hoteli ya Girrafe Ocean View Mbezi Beach jijini Dar es salaam, katikati ni afisa mwandamizi wa Baraza la Sanaa nchini Rawlence Hinju na mwisho kushoto ni Miss Tanzania Miriam Gerald.

Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi (kushoto) akishikana mikono na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Herman Mwansoko wakati wa hafla ya uzinduzi wa semina ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali jana. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Miss Tanzania Dk Ramesh Shah na Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.



Baadhi ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa katika semina yao katika Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Jackson Kalikumtima wakala wa Miss Ilala, Ben Kisaka wakala wa Miss Temeke na Asmah Makau mwandaaji wa Miss Tanga.



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP