Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, March 29, 2010

Wachina Ikulu

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng mara baada ya kuwasili Ikulu leo jijini Dar es salaam kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51.
Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam leo asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP