Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, March 16, 2010

Rais Kikwete Aapisha Katibu Mtendaji Na Manaibu Makatibu Wa Tume Ya Mipango


Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amewaapisha Katibu Mtendaji wa tume ya Mipango na manaibu katibu watendaji wanne wa Tume hiyo. Katika hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Rais amemwapisha Dr.Philip Isdor Mpango kuwa katibu Mtendaji wa tume hiyo na manaibu wake wanne akiwamo Bwana Maduka Paul Kessy, Bi.Happiness Mgalula, Bi.Florence Maridadi Mwanri na Bwana Klifford Katondo Tandari.Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dr.Philip Mpango akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.



Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zana za kazi Naibu Katibu Mtendaji waTume ya Mipango, Clifford Tandari mara baada ya kumwapisha Ikulu jana asubuhi jijini Dar es Salaam.Picha na freddy Maro/Ikulu

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP