WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA VITABU
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiangalia vitabu mbalimbali vya sayansi vilivyotolewa kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia elimu ya Sayansi nchini.Kulia ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.
Wakuu wa vyuo na shule mbalimbali za Sayansi nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya sayansi za maabara kutoka kwa watu wa marekani jana jijini Dar es salaam.Vitabu 1920 vyenye thamani ya shilingi milioni 91 vimetolewa na kukabishiwa kwa wakuu wa vyuo hivyo.
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa chuo cha maabara Litembo kilichoko wilayani Mbinga mkoani Ruvuma sista Angelina Marry Kihwili vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa jana jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi na Afya nchini.Katikati ni mwakilishi wa USG PEPFAR kutoka Marekani Dkt. John Grove.
Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Mkuu wa shule za maabara za Sayansi, Muhimbili Mr. Colman Msuya vitabu vya maabara za Sayansi vilivyotolewa jana jijini Dar es salaam kwa msaada wa Watu wa Marekani kusaidia shule na vyuo mbalimbali vya sayansi nchini.
0 comments:
Post a Comment