Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Wednesday, March 17, 2010

WAZEE WA KABILA LA KIHEHE NA MAKARIBISHO YA MAKAMU WA RAIS MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN, akiwa amekalia Kigoda huku akishikilia Mkuki mara baada ya kuvalishwa Vazi la Utawala wa Kabila la Kihehe na Wazee wa kabila hilo.


Kiongozi wa Kabila la Kihehe katika kijiji cha Mafinga Wilayani Mufindi Mzee SIKAUKA MWACHANGU, akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN baada ya kumvalisha Vazi la Utawala wa Kabila la Kihehe na kumkabidhi Utawala wa Kabila hilo katika Uwanja wa Mashujaa Mafinga Wilayani Mufindi kwa ajili ya kuhutubia Wananchi Mkutano wa Hadhara.

Mzee SIKAUKA MWACHANGU (shoto) na Mzee RAFAEL NGOGO (kuume) ambao ni kati ya Viongozi wa Kabila la Kihehe katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wakimvalisha mgolole, Vazi rasmi la Utawala wa kabila la Kihehe na kumkabidhi Utawala wa Kabila hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN alipowasili katika uwanja wa Mashujaa Mufindi kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara. Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. MOHAMED ABDULAZIZI.

Mzee SIKAUKA MWACHANGU (shoto) na Mzee RAFAEL NGOGO (kuume) ambao ni kati ya Viongozi wa Kabila la Kihehe katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wakimvalisha mgolole, Vazi rasmi la Utawala wa kabila la Kihehe na kumkabidhi Utawala wa Kabila hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN alipowasili katika uwanja wa Mashujaa Mufindi kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara. Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo. Picha na Amour Nassor



0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP