Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Monday, August 31, 2009

Read more...

JK NDANI YA LIBYA

Rais JK akipokewa na waziri wa kilimo na mifugo wa Jamhuri ya Libya Aboubakari Mansoor mara tu baada ya kuiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi jijini Tripoli , rais yuko libya kuhudhuria kikao cha siku moja cha wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika leo 31 .8.09 kuzungumzia masuala ya usalama barani afrika na baadaye kuhudhuria sherehe za miaka 40 ya utawala wa Rais Muammar Gadafi.

Read more...

Shein ndani ya Geneva

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Gavana mkuu wa Geneva David Hiler katika chumba maalum cha kupumzikia wageni alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa mjini Geneva leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano mkuu wa tatu wa kimataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa Duniani unaotarajiwa kuanza kesho mjini Geneva. Katikati Mama Mwanamwema Shein

Read more...


Rais Jakaya Kikwete akiagana na mmoja wa watawa wa Kanisa Katoliki mara baada ya kumalizika kwa futari ambayo aliwaandalia viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, Ikulu, Dar es Salaam juzi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar Es Salaam, Mhashamu Method Kilaini, mara baada ya kumalizika kwa shughuli ya futari ambayo Rais Kikwete aliwaandalia viongozi wa dini na madhehebu mbali mbali nchini juzi, Jumamosi, Ikulu, Dar Es Salaam.

Read more...

Jangili anaswa na nyara

Askari wa wanyama poli katika mbuga ya wanyama ya Wami-Mbiki iliyopo mkoa wa Morogoro na Pwani, Lucas Peter (51) kushoto akitoa minofu ya nyama baada ya jangiri Kaburu Yamungu Moshi kukamatwa na askari hao katika kijiji chaKidudwe wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akidaiwa kuwinda kinyume na sheria. Picha na Juma Mtanda

Read more...

BODI YA UKAGUZI WA FILAMU YAZINDULIWA, UONESHAJI HOLELA WA SINEMA SASA MARUFUKU


Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Pof.Hermas Mwansoko,akifuatiwa na Beneventus Lopa Afisa Mipango na Utawala wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Clement Mshana


Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu mara baada ya uzinduzi.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. Rose Sayore. Picha na habari na Aron Msigwa- MAELEZO.

Read more...

Ajira ya CloudsTV, watu kibao


mtangazaji wa Clouds 88.4 Zamaradi akiwa hoi bin taaban kwa kazi za kufanyia intavyuu mamia ya vijana waliojitokeza kuwania nafasi moja ya atakayekuwa mtangazaji nambari moja wa kituo kipya ya CloudsTV kinachotarajia kuanza kazi karibuni.




zamaradi akiongea na vijana kwenye foleni ya mwisho ya intavyuu. foleni zilikuwa tatu. ya kwanza kupatiwa namba. ya pili kusajili jina na wasifu, ya tatu ni hii



crew wa CloudsTV




vijana wakijiandikisha kabla ya intavyuu

Read more...

Saturday, August 29, 2009

NGOMA AFRICA Wanapofunga Mtaa Hamburg Ujerumani



Ras makunja na kikosi chake The Ngoma Africa band,juzi 21-08-2009waliufunga mtaa mrefu katikati ya jiji kubwa la Hamburg,Ujerumani.katika maonyesho ya Alafia -Afrika Festival,na kusababisha ulinzi mkali kuwepo katika onyesho hilo , mbele ya jukwaa kulijaa mashabiki ambao walikuwa wakidai kuwa ngoma africa ni bendi yao ya damu.
Nyuma ya jukwaa kulikuwa kumejaa Polisi ambao nao walisema kuwa baada ya kumalizika onysho hilo lazima Makunja na kikosi chake wasindikizwe na Ulinzi na hakuna mshabiki wa kuwasogelea! hiyo ilikuwa ikimaanisha FFU wa Ngoma Africa chini ya ulinzi wa washabiki na polisi walikuwa salama kabisa.
Poromota wa onyesho hilo aliwatangazia washabiki kabla ya muziki kuanza kuwa "Washabiki wanaombwa kucheza muziki mbele ya jukwaa" tafadhali nyuma ya jukwaa ni sehemu ya ulinzi tuu! jukwaa lipo kati! upande wa mbele washabiki na upande wa nyuma polisi,Ras Makunja na Ngoma Africa yake wamewekwa mtu kati!!



Ras Makunja akiwa na bendi yake Ngoma Africa

Read more...

Hepi Besdei Ya Kuzaliwa Mzee Wa Libeneke
















Read more...

Waraka wa waislam


Watu wakiwania kununua muongozo huo ambapo nakala moja ilikuwa ikiuzwa Sh.2000


Masheikh mbalimbali wakifurahia kijitabu cha Muongozo


Sheikh Ponda Issa Ponda akionesha kijitabu cha muongozo huo kama ishara ya uzinduzi ramsi.


Sehemu ndogo tu ya maelfu ya waisalamu na wasio waislamu waliofurika katika viwanja ya Mnazi mmoja wakisema kwa sauti moja ‘ 2010 hatudanganyiiiiiki’


Sheikh Mussa Kundecha wa shura ya Maimamu, akifungua hafla hiyo




Read more...

Friday, August 28, 2009

Sasatel yatinga kwa Kova


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Sasatel Christian Haeger akikabidhi vifaa mbalimbali vya mawasiliano kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Suleiman Kova katika makabidhiano yaliyofanyika polisi kati jijini Dar es salaam

Read more...

The Government of Tanzania will soon start construction of a monument and a podium


Mr Isdori Shirima the Arusha Regional Commissioner (Right), The Permanent Secretary of the Ministry of Natural Resources and Tourism Dr Ladislaus Komba (second right) and some officials from the Ministry of Tourism listening to the site explanation given by an officer (not in the picture).

The Arusha Regional Commissioner Mr Isdori Shirima opens a curtain to symbolize Zinjanthropus Pedestal Inauguration at Olduvai Gorge in Ngorongoro Conservation Area Arusha Tanzania.

Read more...

Washindi mbalimbali wa TIGO



Kulia ni Meneja promosheni na matangazo wa Tigo Redemtus Masanja akimkabidhi zawadi Rowland Mwakibete mshindi wa kitita cha milioni moja katika promosheni kabambe ya Tigo Kila Mmoja Anashinda wakati wa hafla fupi ya makabidhianao iliyofanyika makao makuu ya Tigo leo mchana.Katika anaeshuhudia ni Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando.












Read more...

Live ya Hasheem ndani Channel 5







Read more...

Serengeti Boys na dozi zake Sudan


Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Vijana U 17, Salleh Ali akidaka mpira langoni kwake huku mshambuliaji wa Ethiopia, Abdelkarim Hassen akiusubiri umtoke. Nyuma ni Hassan Hamisi akimlinda.Timu hizo zilichuana juzi katika mchezo wa kuwania Kombe la Chalenji la Afrika Mashariki na Kati, Tanzania ilishinda 1-0

Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya mika 17 Hamisi Thabititakijaribu kuwatoka walinzi wa timu ya Ethiopia, Tefesse Solomon (kulia). Thabiti aliiwezesha timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Ethiopia.
Taarifa zilizotufikia hivi punde zina pasha timu ya Zanzibar imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kufungwa goli 2-1 na Elitrea katika mchezo wao wa Robo fainali

Read more...

Washukiwa wa NBM Temeke

Jamaa wakiwa chini ya ulinzi mkali





Jamaa wakificha sura zao

Read more...

Thursday, August 27, 2009

sherehe za jeshi la wananchi kutimiza miaka 45


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mh. Wilson Masilingi akipata ufafanuzi kutoka kwa Luten Kanali Anselum Bahati kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na JWTZ kikosi cha Nyumbu wakati wa maonyesho ya miaka 45 ya JWTZ.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange

Baadhi ya wananchi wakijitokeza kuangalia maonesho ya wiki ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kutimiza miaka 45 wakipata maelezo kuhusu silaha za kivita kutoka kwa wataalam wa Jeshi hilo



Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi mara baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam.Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein mwinyi ambaye aliambatana na Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi (wa kwanza kushoto).

Read more...

JK amzika Askofu Mayala

wakuu wakiagana baada ya kumaliza shughuli ya mazishi. Ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete.


Maaskofu wakiomboleza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu Mkuu Jimbo Katoliki la Mwanza Marehemu Mhashamu Antony Mayala wakati wa ibada ya Mazishi iliyofanyika nyumbani kwake eneo la Kawekamo,Mwanza na baadaye kuzikwa katika kanisa kuu la Epifania mjini Mwanza.


Read more...

mama kikwete azindua kampeni ya vodacom foundation ya mwezi mtukufu wa ramadhani


Mama Salma kikwete akiwasili kwenye eneo la tukio jana mjini Bagamoyo tayari kuzindua kampeni ya Vodacom Foundation ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo pamoja na kufuturisha sehemu mbalimbali nchini misaada kibao hutolewa


Mama Salma Kikwete akiwakabidhi vyakula watoto yatima ambao wanaishi katika mazingira magumu msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba(kulia)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare,Wilayani Bagamoyo jana

Mbunge wa Viti Maalum Mh. Kweigr akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare na Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba huko Bagamoyo jana




baadhi ya wanafunzi wa madras katika hafla hiyo










Mama Salma Kikwete akimkabidhi vifaa vya charahani Mwenyekiti wa kikundi cha kina mama wanaolea watoto yatima Bi.Muridhia Bakari msaada huo ulitolewa na Vodacom Foundation katika kampeni yao ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati)Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba,Wilayani Bagamoyo jana.





Read more...

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP