Dullonet Job,Career and Latest Scholarship

Tuesday, March 9, 2010

duka la mavazi la Tanzania mitindo house lazinduliwa

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha CCM,Mh Janeth Mbene akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa duka la Tanzania Mitindo House,lililopo nyuma ya jengo la hospitali ya Kinondoni jijini Dar,hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.


Mbunifu mkongwe wa mavazi hapa Bongo,Mama Asia Idarous Hamsini wa Fabak Fashions akiwa amepozi na watoto wanaolelewa na Tanzania Mitindo House (TMH) mara baada ya kuwakabidhi zawadi zilizotolewa maalum kwa wanawake (wasichana),pamoja na wabunifu wengine wa mavazi, jana jioni wakati wa uzinduzi wa maaluka la mavazi la Tanzania Mitindo House lililopo nyuma ya jengo la Hospitali ya Kinondoni.






Mwenyekiti wa taasisi ya Tanzania Mitindo House Khadija Mwanamboka akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililosheheni mavazi na bidhaa mbalimbali jana jioni,Kinondoni jijini Dar. Picha zaidi pitia hapa http://www.michuzijr.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment

  © Dullonet template by Dullonet.com 2009

Back to TOP