Richa Adhia awa Miss Tanzania India 2010
Balozi wa India Nchini K.V Bhagrat (Kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Samsung Miss India Tanzania Richa Adhia mara baada ya kukamilia kwa uzinduzi huo kulia ni mwandaaji wa shindano hilo nchini Mustafa Hassanali
Richa Adhia kuwakilisha TANZANIA Uwakilishaji wa TANZANIA kwa mara ya kwanza kwenye 19th MISS INDIA WORLDWIDE
Samsung Miss Tanzania India imezinduliwa jana usiku kwa tafrija iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar-es-Salaam.Miss Tanzania India ni jukwaa linalotoa fursa kwa wanawake wa Kitanzania wenye asili ya Kihindi kuweza kushindana kuonyesha urembo na vipaji vyao ambapo mshindi ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kidunia ya Miss India worldwide.
Ikiwa ni mara ya kwanza, Miss Tanzania India imedhaminiwa na Samsung Electronics, kampuni inayoongoza kwenye nyanja ya mawasiliano duniani na hivyo kufanya ipewe kipaumbele kwa kuliitwa kwa jina la Samsung Miss Tanzania India.
“Mshindi wa Samsung Miss Tanzania India mbali na kuitangaza Tanzania kimataifa pia atajihusisha na shughuli za kijamii ikiwa na pamoja na kuchangisha fedha zitazotumika kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania” alisema Bi.Sati Gadhvi msemaji mkuu wa Miss Tanzania India.
“Mwaka huu ikiwa ni mara ya 19 kwa mashindano ya Miss India Worldwide yatakayofanyika tarehe 27 Machi 2010 kwenye ukumbi wa International Convention Centre mjini Durban, Afrika Kusini.
Mrembo Richa Adhia ataipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mashindano hayo” aliongezea Bi. Gadhvi.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga alikuwepo kwenye uzinduzi huo kama mdau wa mambo ya urembo nchini hapa akiongea na maiwaifu wake Mona na Miss Tanzania Miriam Gerald katikati, hata hivyo alisema shindano hilo halihusiani na Miss Tanzania ila kama mdau amealikwa na ameona ni vema akawapa tafu wadau wenzie.
Mwakilishi wa Samsung Miss India Tanzania Richa Adhia akyake ya televisheni aina ya Samsung LCD kutoka kwa Robert Ngeru Kiongozi wa Biashara wa kampuni ya Samsung.
0 comments:
Post a Comment