Siku ya Wanawake
Wajumbe wa kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakishiriki mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu hali ya wanawake.
Mstari wa Mbele kushoto ni Bi Rahma Khamisi,Mkurugenzi Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto.
Katibu Mkuu Bi Rahma Mshangama, wengine ni Mwanaidi Salehe Abdalla, Bi. Mariam Mwafisi Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi Wahida Mohammed, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya JamiiWANAWAKE
Mbunge wa Peramiho na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Jenista Mhagama akifuatilia mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Hali ya Wanawake, kulia kwake ni Mkurugenzi wa jinsia, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bw Mechack Meliyo Ndaskoi
Dkt. Getrude Mongela akiwasalimia wajumbe wa mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake baada ya kutambuliwa mbele ya wajumbe hao ambao walimshangilia kwa nguvu. Getrude Mongela alikuwa Katibu Mkuiu wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing-China, mkutano huu wa 54 unafanyika ikiwa ni miaka kumi na tano tangu kufanyika kwa mkutano wa Beijing mwaka 1995.
0 comments:
Post a Comment