MWANGUNGA ATAKA WATANZANIA WANUFAIKE NA MALIASILI ZAO NDANI YA UTANDAWAZI
KATIBU MKUU wa wizara ya maliasili na utalii dkt Ladislaus Komba akitoa speech mbele ya bosi wake Shamsa Mwangunga pamoja na mambo mengine akamwambia bosi wake ya kwamba watahakikisha wizara hiyo inachangia zaidi katika pato la taifa kutoka asilimia 17 ya mchango wao kwa sasa
WAZIRI wa maliasili na utalii Shamsa Mwangunga akiwahutubia watendaji wa kada mbalimbali wa wizara hiyo katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika mjini Morogoro pamoja na mambo mengine amewaagiza watendaji hao kuhakikisha watanzania wananufaika na maliasili na utalii ndani ya mfumo wa utandawazi
Bi. Mwangunga amesema ni ukweli kuwa umaskini na utandawazi ni vitu ambavyo havihusiani hata kidogo,kwani wakati umaskini unategemea misaada, utandawazi kwa upande wake unashindanisha ujuzi na maarifa zaidi hivyo wanaotegemea hisani wanadhoofika na kushindwa kunufaika na mfumo huo.
Akasema aka km ndivyo basi watendaji hao wabuni mikakati na mbinu mpya zaidi zitakazowawezesha watanzania ambao wengi wao ni maskini wanufaike na maliasili zao!
0 comments:
Post a Comment