USAID YATOA PIKIPIKI 15 KWA AJILI YA MATIBABU KWA WAATHIRIKA WA UKIMWI
MMOJA wa maafisa wakijaribu pikipiki hizo mbele ya hadhara kuona km zina kiwango stahiki, ama kweli zinafaa jamaa alijinasibu baada ya kujaribu na kuanza safari ya kuelekea hospitali ya berega huko Gairo wilayani Kilosa mkoani Morogoro
Kaimu Afisa Tawala wa mkoa wa Morogoro Steven Bushiri akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki hizo,hafla hiyo ilifanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo amewataka maafisa afya waliokabidhiwa kwenda kutendea kazi zilizolengwa!
Mdada huyu aliyebainika kuwa mmoja wa vinala wa mradi wa tunajali akiweka funguo za pikipiki hizo muda mfupi kabla ya uzinduzi
MGANGA mkuu wa mkoa wa Morogoro dkt Frida Mukiti akishukuru msaada wa USAID kupitia mradi wake wa TUNAJALI kwa msaada wa pikipiki hizo ambazo sasa zimefikia 78 na thamani ya shilingi milioni 320. tukutuku hizo zimegawiwa katika vituo vya afya vilivyopo katika mikoa ya Morogoro, singida,iringa na Dodoma. Picha zote na Nickson Mkilanya wa Bongo Ndiyo Home
0 comments:
Post a Comment