Tahadhari Iringa
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Mohamed Abdulaziz ameuagiza uongozi wa shule ya sekondari ya Iwawa ya wilayani Makete mkoani Iringa kuongeza milango ya tahadhari kwenye bweni jipya la wasichana la shule hiyo.
Pamoja na agizo hilo ametaka wanafunzi watakaoishi katika bweni hilo wawe wale tu ambao idadi yao italingana na uwezo wa bweni hilo.
Alitoa agizo hilo juzi wakati akiweka jiwe la msingi la bweni hilo, ikiwa ni siku chache tu tangu maafa makubwa ya wanafunzi wa kike 12 wa shule ya sekondari ya Idodi, Iringa Vijijini kutetekea kwa moto.
Wanafunzi hao walikufa moto usiku wa manane wakati mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akijisomea kwa kutumia mshumaa, kupitiwa na usingizi kabla moto wa mshumaa huo haujashika chandarua na godoro lake na kwa haraka kutapakaa katika bweni zima la wanafunzi hao lililokuwa na mlango mmoja tu wa kuingilia na kutokea.
0 comments:
Post a Comment